UN: Huenda uchaguzi usifanyike DRC
- 15 Julai 2016
Rais
Kabila anamaliza muda wake mwishoni mwa Desemba mwaka huu
Kiongozi wa tume ya Umoja wa Mataifa
kuhusiana na masuala ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amenukuliwa akisema
nchi hiyo huenda isiweze kuandaa uchaguzi wa urais hapo Novemba kama ilivyokuwa
imepangwa.
Akitoa matamshi hayo asubuhi ya leo,
kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters,
Kwa mujibu wa shirika la habari la
Reuters, mkuu wa tume hiyo Maman Sidikou ameambia kikao cha waandishi habari
mjini Kinshasa kwamba ''ni raia wa Congo wenyewe ambao wataamua ni lini
uchaguzi huo utakapofanyika'.
Maafisa kadhaa katika Umoja wa
Mataifa wamekuwa wakionya kwamba kucheleweshwa kwa uchaguzi huo huenda kukazua
upya vurugu na rabsha za kisiasa nchini humo.
Rais Joseph Kabila anatarajiwa
kuondoka madarakani baada ya muhula wake kukamilika.
Hata hivyo, wapinzani wake wasema
anachelewesha uchaguzi huo wa Novemba 27 kimakusudi ili aendelee kusalia
mamlakani.
BBC SWAHILI
BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment