Santos achaguliwa tena kuongoza chama tawala Angola
Rais wa Angola, Jose Eduardo dos
Santos aliyeongoza kwa miaka 36 amechaguliwa tena kuwa kiongozi wa chama tawala
cha MPLA.
Uchaguzi wa bunge unatarajiwa
kufanywa mwaka ujao, na kiongozi wa chama kinachoshinda ndiye anayekuwa rais.
Rais dos Santos alisema awali mwaka
huu, kwamba ataondoka madarakani mwaka wa 2018, lakini ameshawahi kutoa ahadi
kama hizo kabla.
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka
73, analaumiwa kuwa amekusanya madaraka mengi na mali, kwenye mikono ya familia
yake na washirika wake wakubwa kisiasa.
BBC SWAHILI 20 / 08 / 2016
No comments:
Post a Comment