Rais wa Zambia aapishwa kwa muhula mwingine
- 13 Septemba 2016
Lungu alipata asilimia
50.35 ya kura zilizopigwa
Rais wa Zambia Edga Lungu ameapishwa
hii leo baada ya kuchaguliwa tena wakati wa uchaguzi wa mwezi Agosti.
Kuapishwa kwake kunafanyika baada ya
upinzani kushindwa katika kesi ya kutaka matokeo ya uchaguzi kubatilishwa.
Mwandishi wa BBC
anasema kuwa takriban watu 60,000 wamefika kushuhudia kuapishwa kwa Rais Lungu
Mahakama ya katiba ilitupilia mbali
kesi ikisema kuwa upinzai ulikuwa umeishiwa muda wa kupeleka suala hilo
mahakamani.
Bwana Lungu alishinda uchaguzi wa
tarehe 11 mwezi Agosti kwa asilimia 50.35 na kupita kiwango kilichokwa kuepuka
kurudiwa tena kwa uchaguzi.
Mgombea wa upinzani
Hakainde Hichilema alishindwa kubatilisha matokeo ya uchaguzi mahakamani
Hakainde Hichilema ambaye alichukua
nafasi ya pili kwa asilimia 47.63 anaendelea kupinga matokeo hayo.
Mwandishi wa BBC aliye kwenye uwanja
wa National Heroes katika mji mku wa Zambia Lusaka, anasema kuwa takriban watu
60,000 wamefika kushuhudia kuapishwa kwa Rais Edga Lungu.
BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment