Mfalme wa Thailand Bhumibol Adulyadej afariki dunia
akiwa na miaka 88
- 13 Oktoba 2016
Mfalme wa Thailand Bhumibol
Adulyadej, mfalme aliyetawala kwa muda mrefu zaidi duniani, amefariki dunia
akiwa na umri wa miaka 88, kasri kuu nchini humo imetangaza.
Alikuwa ametawala kwa miaka 70.
Mfalme huyo alienziwa sana nchini
Thailand na amekuwa akitazamwa kama nguzo kuu ya kuunganisha taifa hilo ambalo
limekumbwa na misukosuko mingi ya kisiasa na mapinduzi ya serikali.
Alikuwa amedhoofika sana kiafya
miaka ya karibuni na hajakuwa akionekana hadharani sana.
Kifo chake kimetokea huku Thailand
ikisalia chini ya utawala wa kijeshi kufuatia mapinduzi yaliyotekelezwa 2014.
Ikulu ilikuwa awali imeonya kwamba
hali yake ya afya ilikuwa imedhoofika zaidi Jumapili.
Raia
walikuwa wamekusanyika nje ya hospitali alimolazwa kumtakia heri
Raia wa Thailand wamekuwa wakivalia
mavazi ya rangi ya waridi kumtakia heri.
Mamia walikusanyika nje ya hospitali
ambapo alikuwa akitibiwa.
Anayetarajiwa kumrithi Mfalme
Bhumibol ni Mwanamfalme Vajiralongkorn, 63, ambaye huwa havutii watu sana kama
babake.
Sheria kali kuhusu familia ya
kifalme nchini humo huzuia umma kujadili masuala ya urithi hadharani.
Ukipatikana na kosa hilo unaweza kufungwa jela muda mrefu.
Ikizingatiwa mchango muhimu
aliotekeleza mfalme huyo kuhakikisha uthabiti wa kisiasa nchini Thailand, suala
la mrithi wake litakuwa changamoto kuu kwa serikali, anasema mwandishi wa BBC
aliyeko Bangkok Jonathan Head.
King Bhumibol, alizaliwa Cambridge
katika jimbo la Massachusetts, nchini Marekani.
Alitawazwa mfalme tarehe 9 Juni 1946
baada ya kifo cha kakake Mfalme Ananda Mahidol.
Ingawa mfalme kikatiba nchini humo
hana mamlaka makubwa, Mfalme Bhumibol alitazamwa na wengi kama mfalme
aliyetawazwa na Mungu.
Mfalme
Bhumibol Adulyadej aliheshimiwa sana Thailand