Bosco Ntaganda: niko tayari kufa
- 13 septemba 2016
Ntaganda
analaumiwa kwa kuwatumia watoto kama wanajeshi, na wanake kama watumwa wa ngono
Kamanda wa zamani waasi nchini
Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, ambaye anakabiliwa na kesi katika mahakama ya
kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC huko Hague, amasema kuwa yuko tayari kufa
badala ya kuvumilia hali anayopitia sasa akiwa kizuizini kwa mjibu wa shirika
la habari ya Reuters.
Bosco Ntaganda ambaye analaumiwa kwa
kuwatumia watoto kama wanajeshi, na wanake kama watumwa wa ngono na pia mauaji
nchini Jamhuri ya Demokrasi Congo kati ya mwaka 2002 na 2003, alianza mgomo wa
kutokula wiki iliyopita.
Ntaganda
anasema hana uwezo wa kumuona mkewe na watoto
"Sina uwezo wa kumuona mke
wangu na watoto tena katika hali nilivyo sasa. Hii ndiyo sababu imenifanya
nipoteze matumani.Ndiyo sababu niko tayari kufa," Ntaganda alisema katika
taarifa iliyosomwa na wakili wake.
Ntaganda alikana mashtaka yote 18
dhidi yake wakati wa kuanza kwa kesi mwaka uliopita.
BBC SWAHILI
BBC SWAHILI