Rais
wa Tanzania John Pombe Magufuli amesema serikali imeamua kusimamisha kwa muda
usiozidi miezi miwili zoezi la utoaji ajira mpya na upandishaji wa vyeo kwa
watumishi wa umma.
Amesema
kuwa hatua hiyo inalenga kuapisha uhakiki wa watumishi wa umma katika orodha ya
malipo ya mshahara na kuondoa watumishi hewa.
Akizungumza
wakati wa kuadhimisha miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania,amesema kuwa hatua hiyo
hailengi kuwakatisha tamaa watumishi wa umaa.
Amesema
kuwa shughuli za kuwaajiri na kuwapansisha veyo maafisa hao itaendelea kama
kawaida baada ya kukamilika kwa zoezi hilo.
"Serikali
ninayoiongoza haina nia ya kuwakatisha tamaa wafanyakazi, lengo lake ni
kujipanga kwa makosa tuliyoyafanya, na ndio maana nimesema kwa kipindi cha
mwezi mmoja hivi au hata mwezi mmoja na nusu, haitazidi miezi miwili, tusiajiri
mtumishi yeyote serikalini, lakini pia katika kipindi cha mwezi mmoja
hatutawapandisha vyeo wafanyakazi.Ninaomba wafanyakazi waelewe hili, kwa sababu
tukiendelea tutakuwa tunawapandisha vyeo hata wafanyakazi ambao hawapo,
tunafanya ukaguzi wote tukishamaliza wafanyakazi wataendelea kupandishwa
vyeo" alisema Rais Magufuli.
Wakati
huo huo,Rais Magufuli ameiagiza Benki Kuu ya Tanzania kuchukua hatua mara moja
dhidi ya benki ambazo hazizalishi faida zikiwemo benki za serikali, kufuta
akaunti mfu na kuanzisha mara moja akaunti moja ya mapato na matumizi ya
serikali .
Maadhimisho
hayo yalihudhuriwa na Magavana na Manaibu Gavana kutoka nchi 18 za Jumuiya ya
Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika (SADC),
Mabalozi kutoka nchi mbalimbali, Viongozi wa Taasisi za fedha za Afrika na
Makatibu wakuu wa Wizara za Fedha na Mipango wa Tanzania Bara na Tanzania
Zanzibar.
BBC SWAHILI, 23/06/2016