Mchango wa Shimon Perez nchini Israel
- Saa 8 zilizopita
Shimon Peres amekuwa kiongozi mkuu
katika maswala ya kisiasa nchini Israel,kwa kipindi chote ambacho taifa hilo
limekuwepo hadi kufikia sasa.
Alishikilia nyadhfa nyingi ,zikiwemo
zile za waziri mkuu na rais,ijapokuwa hakufanikiwa kuongoza chama kushinda
uchaguzi.
Akiwa mzaliwa wa Szymon Perski huko
Wiszniew,Poland ikiwa sasa inaitwa Visnieva ,Belarus, tarehe 2 mwezi Agosti
1923,Shimon Peres alikuwa mwana wa mfanyibiashara wa mbao.
Wazazi wake hawakuwa Wayahudi wa
Kiorthodoksi,lakini kijana huyo alifunzwa maandishi ya sheria za Wayahudi na
babu yake na akawa mfuasi mkubwa wa dini hiyo.
Mwaka 1934,familia yake ilihamia
Palestine,eneo ambalo babake Pirez alikuwa amehamia miaka miwili kabla ya
kwenda kuishi Tel Aviv.
Image caption Shimon Peres,Yitzak
Rabin na Yasser Arafat wakitia saini makubaliano ya amani
Baada ya kwenda katika shule ya
kilimo,Peres alifanya kazi katika kilimo cha jamii na kujihusisha katika siasa
akiwa katika umri wa miaka 18 wakati alipochaguliwa katibu wa vuguvugu la
wafanyikazi wa Kizayuni.
Mwaka 1947,Mwanzilishi wa Israel na
waziri mkuu David Ben Gurion,alimpatia wadhfa wa kusimamia wafanyikazi na
ununuzi wa silaha wa Haganah,mtangulizi wa jeshi la Israel.
Alipata mpango na Ufaransa
kulinunulia jimbo hilo jipya ndege za kivita na kuanzisha ujenzi wa siri wa
kituo cha Kinyuklia katika eneo la Dimona.
Perez alichaguliwa katika bunge la
Israel mwaka 1959,akigombea kupitia tiketi ya chama cha Mapai,ana akateuliwa
kuchukua wadhfa wa naibu waziri wa ulinzi nchini humo.
Mnamo mwaka 1965,alijiuzulu baada ya
kudaiwa kuanzisha operesheni Susannah,mpango wa kuyalipua maeneo ya Uingereza
na Marekani nchini Misri mwaka 1954 kwa lengo la kuishinkiza Uingereza
kutoondoa vikosi vyake kutoka eneo la Sinai.
Uchunguzi kuhusu mpango huo
haukupata ukweli wowote ,na hapo ndiposa Peres,pamoja na Ben Gurion,alikihama
chama cha Mapai na kuanzisha chama kipya.
Wakati Golda Meir alipojiuzulu kama
waziri mkuu mwaka 1974 baada ya vita vya Yom Kippur ,Peres hakufanikiwa
kukabiliana na Yitzhak Rabin kuchukua kiti hicho kilichokuwa wazi.
- Majadiliano ya siri
Rabin alisimama kama kiongozi wa
chama cha Alignment Party mwaka 1977 baada ya kashfa ya sarufi iliomuhusisha
mkewe ,lakini kutokana na pengo lililokuwepo katika sheria hakuweza kujiuzulu
kama waziri mkuu.
Peres baadaye alikuwa kiongozi wa
chama na waziri mkuu asiye rasmi kabla ya kuuongoza muungano huo ulioshindwa na
chama cha Likud chini ya uongozi wa Menachem Begin.
Alishindwa katika chaguzi
kadhaa,zote akipewa nyadhfa za waziri kama mpango wa serikali ya muungano.
Mwaka 1992,Peres alishindwa kushinda
uongozi wa chama cha Leba nchini Israel baada ya kushindwa katika awamu ya
kwanza ya uchaguzi na Rabin.
Image caption Chama cha Leba ndicho
kilichopigania maelewano katika eneo la West Bank
Akiwa waziri wa maswala ya kigeni wa
serikali ya Rabin ,Peres alianza majadiliano ya siri na Yasser Arafat na chama
cha PLO,ambayo yalisasababisha makubaliano ya amani ya Oslo mwaka 1993.
Kwa mara ya kwanza uongozi wa
Palestina ulitambua uwepo wa taifa la Israel na haki zake.Mwaka mmoja baadaye
Peres,Rabin na Arafat walishinda tuzo la pamoja la amani la Nobel.
Wakati mmoja akiwa mtetezi wa
makaazi ya Wayahudi huko West Bank ,Peres alikuwa mpatanishi ,kila mara
akizungumzia umuhimu wa maelewano kuhusu mahitaji ya Palestina katika eneo
hilo.
''Wapelestina ni majirani zetu
wakubwa'' ,alisema wakati mmoja.''Ninaamini watakuwa marafiki zetu''.
Peres aliwahi kuwa waziri mkuu mwaka
1995 baada ya mauaji ya Rabin ,lakini alishikilia afisi hiyo chini ya mwaka
mmoja kabla ya kushindwa na Benjamin Netanyahu wa chama cha Likud.
- Maridhiano
Mwaka 2000,alishindwa katika juhudu
zake kuchukua wadhfa wa rais asiye na mamlaka ,baada ya kushindwa na Moshe
Katsav.
Baada ya mrithi wake kiongozi wa
chama cha Leba ,Ehud Barak kushindwa na Ariel Sharon katika uchaguzi wa mwaka
2002,Peres alikiongoza chama cha Leba kufanya muungano na Likud na kuzawadiwa
afisi ya waziri wa maswala ya kigeni.
Mwaka 2005,Peres alitangaza
kujiuzulu kwake katika chama cha Leba pamoja na kumuunga mkono Sharon ambaye
alikuwa ameanzisha chama cha Kadima.
Image caption Benjamin Netanyahu
alikuwa waziri mkuu huku mpinzani wake Shimon Peres akiwa rais
Baada ya Sharon kuugua
kiharusi,kulikuwa na uvumi kwamba Peres angekuwa kiongozi wa Kadima lakini
alizuiwa na wanachama wa chama cha Likud ambao walikuwa wengi katika chama.
Mnamo mwezi Juni mwaka
2007,alichaguliwa rais wa Israel,na kujiuzulu katika bunge ambapo alikuwa ndiye
kiongozi aliyehudumu kwa mda mrefu katika historia ya taifa hilo.
Alihudumu kwa miaka saba kama rais,kabla
ya kujiuzulu mwaka 2014,akiwa rais mwenye umri mkubwa duniani.