Image caption Rais Uhuru Kenyatta
Rais
wa Kenya Uhuru Kenyatta amesisitiza kuwa serikali haitaruhusu maandamano ya
ghasia akitaja yale yanayofanywa na chama cha Upinzani Cord ambayo yamegeuka na
kuwa maandamano na maafisa wa polisi.
Lakini
aliongezea kuwa wataruhusu maandamano iwapo yatasalia kuwa ya amani kama ilivyo
katika katiba.
Upinzani
wa Cord umekuwa akifanya maandamano mara kwa mara ukitaka mabadiliko katika
tume ya uchaguzi.
Awali
siku ya Ijumaa upinzani huo umesema utakiuka agizo la waziri wa usalama la
kupiga marufuku maandamano.
Bw
Kenyatta ameutaka upinzani kuzungumza na serikali kuhusu maswala
muhimu.''Tumetengeza timu... yetu leteni yenu'',alisema.
CHANZO CHA HABARI: BBC SWAHILI , 10 JUNI 2016