Wednesday, June 15, 2016

MGOMBEA URAISI WA ZAMANI AKAMATWA CONGO---BRAZZAVILE




 
MICHEL   MOKOKO
Mkuu wa zamani wa jeshi na mgombea wa kiti cha urais aliyeshindwa nchini Congo-Brazzaville amekamatwa

Hakuna sababu iliyotolewa ya kukamatwa kwa jenerali Jean-Marie Michel Mokoko, lakini Rais Denis Sassou Nguesso amemlaumu awali kwa kupanga mapinduzi.

"Hii ni njia ya kumdhuru jenerali, ambaye alisimama na bwana Nguesso wakati wa uchaguzi uliopita," msemaji wa chama cha I'IDC-FROCAD Guy Romain Kinfouissia , aliliambia shirika la Reuters.

Bwana Sassou Nguesso ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1979, alichaguliwa tena mwezi Machi kwenye uchaguzi uliopingwa na upinzani.

BBC   SWAHILI , 15/06/2016