Saturday, August 20, 2016

ALIYEMWITA " MBWA WAKE BUHARI " AACHILIWA HURU



Aliyemwita ''mbwa wake Buhari'' aachiliwa huru
  • 18 Agosti 2016
Mwanamume mmoja wa Nigeria aliyekamatwa kwa kumuita mbwa wake jina la rais Muhamadu Buhari amewachiliwa huru bila ya kushtakiwa,kulingana na chombo cha habari cha Vanguard.
Joe Fortemose Chinakwe aliambia mtandao huo kwamba hakuwa na lengo la kumtusi rais alipomtaja mbwa wake jina la rais huyo.
Amesema kwake anaona kwamba ni sifa kubwa kwa kuwa anapendelea maamuzi ya rais huyo.

''Nilimuita mbwa wangu jina la rais kwa kuwa yeye ni shujaa wangu.Nilianza kumpenda Buhari wakati alipokuwa rais mwanajeshi hadi leo ambapo amekuwa raia.Baada ya kusoma kuhusu maamuzi yake dhidi ya ufisadi unaokula uchumi wa taifa hili ,niliamua kulibadilisha jina la mbwa wangu ambye nilimuita Buhari.Sikujua kwamba nilikuwa nafanya makosa kwa kumpenda Buhari''. 
 
Image caption Muhammadu Buhari