Image copyright Getty Image caption Obama
ataanza kufanya kampeni na Clinton
Rais
wa Marekani Barack Obama ametangaza kumuunga mkono Hillary Clinton kuwa mgombea
urais wa chama cha Democratic katika uchaguzi mkuu utakaofanyika baadaye mwaka
huu nchini Marekani.
Amechukua
hatua hiyo muda mfupi baada ya kukutana na seneta wa Vermont Bernie Sanders
ambaye amekuwa akikabiliana na Bi Clinton katika kinyang’anyiro cha kumchagua
mgombea wa chama hicho.
Akizungumza
kwenye video ambayo imepakiwa kwenye Twitter na Bi Clinton, Bw Obama amesema
mgombea huyo ndiye aliyewahi kuhitimu zaidi kuwa rais wa Marekani.
“Niko
pamoja naye, nina msisimko na nasubiri sana kutoka huko nje na kufanya kampeni
na Hillary,” amesema Obama.
Obama alikutana na Sanders ikulu ya White House
Wawili
hao sasa wanatarajiwa kuanza kufanya kampeni pamoja.
Bw
Sanders naye amesema yuko tayari kufanya kazi na mpinzani wake, Bi Clinton,
kumshinda mgombea wa chama cha Republican Donald Trump katika uchaguzi mkuu.
Hata
hivyo hakujiondoa kinyang’anyironi. Alisema ataendelea kufanya kampeni yake na
kwamba anatumai atakutana na Bi Clinton hivi karibuni.
CHANZO CHA HABARI: BBC SWAHILI , 09/06/ 2016
No comments:
Post a Comment