Tuesday, September 13, 2016

RAIS WA ZAMBIA AAPISHWA KWA MUHULA MWINGINE



Rais wa Zambia aapishwa kwa muhula mwingine
  • 13 Septemba 2016
 Lungu alipata asilimia 50.35 ya kura zilizopigwa
Rais wa Zambia Edga Lungu ameapishwa hii leo baada ya kuchaguliwa tena wakati wa uchaguzi wa mwezi Agosti.
Kuapishwa kwake kunafanyika baada ya upinzani kushindwa katika kesi ya kutaka matokeo ya uchaguzi kubatilishwa.
 Mwandishi wa BBC anasema kuwa takriban watu 60,000 wamefika kushuhudia kuapishwa kwa Rais Lungu 
 
Mahakama ya katiba ilitupilia mbali kesi ikisema kuwa upinzai ulikuwa umeishiwa muda wa kupeleka suala hilo mahakamani.
Bwana Lungu alishinda uchaguzi wa tarehe 11 mwezi Agosti kwa asilimia 50.35 na kupita kiwango kilichokwa kuepuka kurudiwa tena kwa uchaguzi.

Mgombea wa upinzani Hakainde Hichilema alishindwa kubatilisha matokeo ya uchaguzi mahakamani 

Hakainde Hichilema ambaye alichukua nafasi ya pili kwa asilimia 47.63 anaendelea kupinga matokeo hayo.
Mwandishi wa BBC aliye kwenye uwanja wa National Heroes katika mji mku wa Zambia Lusaka, anasema kuwa takriban watu 60,000 wamefika kushuhudia kuapishwa kwa Rais Edga Lungu.

BBC   SWAHILI

No comments:

Post a Comment