Upinzani waandamana dhidi ya rais Kabila DRC
- 19 Septemba 2016
Waandamanaji wameweka vizuizi na
kuchoma magari katika mji mkuu wa Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo,baada ya maafisa wa polisi kuwazuia kuandamana.
Wanamtaka rais Joseph Kabila
ajiuzulu baada ya kukamilika kwa muhula wake mnamo mwezi Disemba tarehe 20 kulingana
na mwandishi wa BBC Poly Muzalia.
Chombo cha habari cha reuters
kiliwanukuu mashahidi wakisema kuwa maafisa wa polisi walifyatua risasi
kuwatawanya waandamanaji.
Upinzani unahofia kwamba bwana
Kabila ana mpango wa kuchelewesha uchaguzi wa urais unaotarajiwa mwezi Novemba
ili kusalia madarakani.
Maafisa wa uchaguzi na serikali
wanasema kuwa uchaguzi huo utaahirishwa kutokana na matatizo ya mipango katika
taifa hilo la Afrika ya kati.
Taifa la DRC halijawahi kuwa na
ukabidhi wa mamlaka ulio huru tangu uhuru wake zaidi ya miaka 45 iliopita.
Waandamanaji wakiweka vizuizi na kuchoma
moto katika barabara za Kinshasa
No comments:
Post a Comment