Ufaransa yatishia kuiwekea vikwazo DRC
04/10/2016
Rais
Joseph Kabila wa DRC
Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya
Congo ,Joseph Kabila ni sharti aheshimu katiba na kujiuzulu mwishoni mwa muhula
wake ,waziri wa maswala ya kigeni nchini Ufaransa Jean-Mark Ayrault amesema
katika mahojiano na kituo cha habari cha TV5.
Bwana Ayrault alikuwa akisisitiza
wito aliotoa wiki iliopita wakati akiwahutubia wanafunzi mjini Paris.
Wakati huu aliangazia madai kwamba
Ufaransa imekuwa ikiingilia maswala ya ndani ya DRC,akisema kuwa taifa lake
haliko pekee kumkumbusha Kabila kwamba lazima aheshimu sheria.
Aliambia kituo hicho: ''Rais Kabila
lazima aonyeshe mfano mwema. Ni lazima aheshimu katiba. Iwapo vikwazo
vitahitajika tutaamua kuvitekeleza. Nataka watu waelewe; Watu waliopo katika
mamlaka DRC ni lazima wawajibike. Iwapo wanahitaji amani nchini mwao, iwapo
wanajali hali ya watu wao ,ni lazima wafuate katiba''.
Lakini serikali ya DRC imesema
Ufaransa inachochea maasi dhidi ya serikali nchini humo.
Waziri wa mawasiliano Lambert Mende
ameambia shirika la habari la AFP kwamba Ufaransa 'inacheza mchezo hatari'.
"Baada ya kuwasha moto na
kuwahimiza watu wenye misimamo mikali, Ufaransa itawaondoa raia wake na
kuwaacha raia wa Congo taabani," ameambia wanahabari.
"Wasiwasi wa Waziri Ayrault
kuhusu DRC unazua shaka kwa sababu unafufua kumbukumbu za uingiliaji kati ambao
ulizaa vurugu Libya."
No comments:
Post a Comment