MICHEL MOKOKO
Mkuu
wa zamani wa jeshi na mgombea wa kiti cha urais aliyeshindwa nchini
Congo-Brazzaville amekamatwa
Hakuna
sababu iliyotolewa ya kukamatwa kwa jenerali Jean-Marie Michel Mokoko, lakini
Rais Denis Sassou Nguesso amemlaumu awali kwa kupanga mapinduzi.
"Hii
ni njia ya kumdhuru jenerali, ambaye alisimama na bwana Nguesso wakati wa
uchaguzi uliopita," msemaji wa chama cha I'IDC-FROCAD Guy Romain
Kinfouissia , aliliambia shirika la Reuters.
Bwana
Sassou Nguesso ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1979, alichaguliwa tena
mwezi Machi kwenye uchaguzi uliopingwa na upinzani.
BBC SWAHILI , 15/06/2016
No comments:
Post a Comment