TRUMP
Rais
wa Marekani, Barack Obama, ameshtumu vikali matamshi ya mgombea urais kwa
tiketi ya chama cha Republican, Donald Trump, kwamba waislamu wasiruhusiwe
kuingia Marekani. Obama amesema hiyo 'si marekani wanayohitaji."
''Kuwabagua
Waislamu wa Marekani kutasababisha nchi hiyo kukosa usalama,na kuongeza tofauti
iliopo kati ya nchi za magharibi na zile za kislamu'', Obama alisema
Siku
ya Jumatatu bwana Trump, aliongezea kuhusu mpango wa kupiga marufuku nchi zote
ambazo zina historia ya kutekeleza mashambulizi dhidi ya Marekani.
Alisema
shambulio la ufyatuliaji risasi la Orlando linathibitisha yote.
Watu
49 waliuawa, baada ya Omar Mateen raia wa Marekani ambaye wazazi wake ni raia
wa Afghan kufyatua risasi katika kilabu ya wapenzi wa jinsia moja huko Orlando.
Bwana
Trump amesema pendekezo lake litatekelezwa kupitia (uamuzi wa pamoja ) iwapo
rais atapewa mamlaka ya kupiga marufuku uingizaji wa watu wenye daraja lolote
katika nchi hiyo jambo ambalo rais ataliona kuleta madhara ya kiusalama kwa
Marekani.
Lakini
siku ya Jumanne katika wizara ya fedha mjini Washington,Obama aliyekuwa
amekasirishwa na matamshi hayo ya Trump alimshambulia mgombea huyo
anayetarajiwa kuthibitishwa kuwa mteuzi wa urais wa chama cha Republican mwezi
ujao.
No comments:
Post a Comment