Jaji
nchini Uganda ametoa amri kuwa kesi ya kiongozi wa upinzani nchini humo Kizza
Besigye, ifanyike mahakamani kwa makosa ya uhaini na wala sio kwenye gereza
lenye ulinzi mkali ambapo anazuiliwa.
Besigye
alifikishwa mahakamani kwa muda mfupi ambapo kesi yake iliahairisha hadi tarehe
29 mwezi Juni.
Mwendesha
mashtaka aliomba kesi hiyo kufanyika mahakamani kutokana na sababu za
kiusalama.
Alikamatwa
mwezi uliopita na kushtakiwa kwa uhaini baada ya kupanga sherehe za kuapishwa
kwake kama rais.
Alipinga
ushindi wa Rais Yoweri Museveni wa awamu ya tano wa uchaguzi wa mwezi Februari.
BBC, SWAHILI , 15/06/2016
No comments:
Post a Comment