Afya ya Shimon Perez wa Israel yazorota
- 28 Septemba 2016
Taarifa kutoka nchini Israel
zinaeleza kuwa afya ya mwanasiasa mkongwe na waziri Shimon Peres imezorota mno
.Ndugu wa karibu wakiongozi huyo wa zamani ndiyo wenye ruhusa ya kwenda katika
hospitalia aliyolazwa yapata wiki mbili zilizopita kutokana na tatizo la
kushambuliwa na kiharusi mara kadhaa.
Ikumbukwe kwamba Shimon Peres
ameitumikia nchi hiyo kama waziri mkuu mara mbili na mara moja katika nafasi ya
Rais.Simon pia aliwahi kutunukiwa tuzo ya amani ya Nobel kwa ushiriki wake
mkubwa katika harakati za kutafuta suluhu ya mgogoro wa kisiasa baina ya Israel
na Palestina mnamo miaka ya 1990.
Shimon Perez ni miongoni mwa kizazi
cha mwisho cha wanasiasa walioshuhudia kuzaliwa kwa taifa jipya la Israel mnamo
mwaka 1948 .
BBC SWAHILI
Shimon Perez
No comments:
Post a Comment