Wednesday, September 28, 2016

MCHANGO WA SHIMON PEREZ NCHINI ISREL




Mchango wa Shimon Perez nchini Israel
  • Saa 8 zilizopita

Shimon Peres amekuwa kiongozi mkuu katika maswala ya kisiasa nchini Israel,kwa kipindi chote ambacho taifa hilo limekuwepo hadi kufikia sasa.
Alishikilia nyadhfa nyingi ,zikiwemo zile za waziri mkuu na rais,ijapokuwa hakufanikiwa kuongoza chama kushinda uchaguzi.

Akiwa mzaliwa wa Szymon Perski huko Wiszniew,Poland ikiwa sasa inaitwa Visnieva ,Belarus, tarehe 2 mwezi Agosti 1923,Shimon Peres alikuwa mwana wa mfanyibiashara wa mbao.
Wazazi wake hawakuwa Wayahudi wa Kiorthodoksi,lakini kijana huyo alifunzwa maandishi ya sheria za Wayahudi na babu yake na akawa mfuasi mkubwa wa dini hiyo.
Mwaka 1934,familia yake ilihamia Palestine,eneo ambalo babake Pirez alikuwa amehamia miaka miwili kabla ya kwenda kuishi Tel Aviv.
Image caption Shimon Peres,Yitzak Rabin na Yasser Arafat wakitia saini makubaliano ya amani
Baada ya kwenda katika shule ya kilimo,Peres alifanya kazi katika kilimo cha jamii na kujihusisha katika siasa akiwa katika umri wa miaka 18 wakati alipochaguliwa katibu wa vuguvugu la wafanyikazi wa Kizayuni.
Mwaka 1947,Mwanzilishi wa Israel na waziri mkuu David Ben Gurion,alimpatia wadhfa wa kusimamia wafanyikazi na ununuzi wa silaha wa Haganah,mtangulizi wa jeshi la Israel.
Alipata mpango na Ufaransa kulinunulia jimbo hilo jipya ndege za kivita na kuanzisha ujenzi wa siri wa kituo cha Kinyuklia katika eneo la Dimona.
Perez alichaguliwa katika bunge la Israel mwaka 1959,akigombea kupitia tiketi ya chama cha Mapai,ana akateuliwa kuchukua wadhfa wa naibu waziri wa ulinzi nchini humo.
Mnamo mwaka 1965,alijiuzulu baada ya kudaiwa kuanzisha operesheni Susannah,mpango wa kuyalipua maeneo ya Uingereza na Marekani nchini Misri mwaka 1954 kwa lengo la kuishinkiza Uingereza kutoondoa vikosi vyake kutoka eneo la Sinai.
Uchunguzi kuhusu mpango huo haukupata ukweli wowote ,na hapo ndiposa Peres,pamoja na Ben Gurion,alikihama chama cha Mapai na kuanzisha chama kipya.
Wakati Golda Meir alipojiuzulu kama waziri mkuu mwaka 1974 baada ya vita vya Yom Kippur ,Peres hakufanikiwa kukabiliana na Yitzhak Rabin kuchukua kiti hicho kilichokuwa wazi.
  • Majadiliano ya siri
Rabin alisimama kama kiongozi wa chama cha Alignment Party mwaka 1977 baada ya kashfa ya sarufi iliomuhusisha mkewe ,lakini kutokana na pengo lililokuwepo katika sheria hakuweza kujiuzulu kama waziri mkuu.
Peres baadaye alikuwa kiongozi wa chama na waziri mkuu asiye rasmi kabla ya kuuongoza muungano huo ulioshindwa na chama cha Likud chini ya uongozi wa Menachem Begin.
Alishindwa katika chaguzi kadhaa,zote akipewa nyadhfa za waziri kama mpango wa serikali ya muungano.
Mwaka 1992,Peres alishindwa kushinda uongozi wa chama cha Leba nchini Israel baada ya kushindwa katika awamu ya kwanza ya uchaguzi na Rabin.
Image caption Chama cha Leba ndicho kilichopigania maelewano katika eneo la West Bank
Akiwa waziri wa maswala ya kigeni wa serikali ya Rabin ,Peres alianza majadiliano ya siri na Yasser Arafat na chama cha PLO,ambayo yalisasababisha makubaliano ya amani ya Oslo mwaka 1993.
Kwa mara ya kwanza uongozi wa Palestina ulitambua uwepo wa taifa la Israel na haki zake.Mwaka mmoja baadaye Peres,Rabin na Arafat walishinda tuzo la pamoja la amani la Nobel.
Wakati mmoja akiwa mtetezi wa makaazi ya Wayahudi huko West Bank ,Peres alikuwa mpatanishi ,kila mara akizungumzia umuhimu wa maelewano kuhusu mahitaji ya Palestina katika eneo hilo.
''Wapelestina ni majirani zetu wakubwa'' ,alisema wakati mmoja.''Ninaamini watakuwa marafiki zetu''.
Peres aliwahi kuwa waziri mkuu mwaka 1995 baada ya mauaji ya Rabin ,lakini alishikilia afisi hiyo chini ya mwaka mmoja kabla ya kushindwa na Benjamin Netanyahu wa chama cha Likud.
  • Maridhiano
Mwaka 2000,alishindwa katika juhudu zake kuchukua wadhfa wa rais asiye na mamlaka ,baada ya kushindwa na Moshe Katsav.
Baada ya mrithi wake kiongozi wa chama cha Leba ,Ehud Barak kushindwa na Ariel Sharon katika uchaguzi wa mwaka 2002,Peres alikiongoza chama cha Leba kufanya muungano na Likud na kuzawadiwa afisi ya waziri wa maswala ya kigeni.
Mwaka 2005,Peres alitangaza kujiuzulu kwake katika chama cha Leba pamoja na kumuunga mkono Sharon ambaye alikuwa ameanzisha chama cha Kadima.
Image caption Benjamin Netanyahu alikuwa waziri mkuu huku mpinzani wake Shimon Peres akiwa rais
Baada ya Sharon kuugua kiharusi,kulikuwa na uvumi kwamba Peres angekuwa kiongozi wa Kadima lakini alizuiwa na wanachama wa chama cha Likud ambao walikuwa wengi katika chama.
Mnamo mwezi Juni mwaka 2007,alichaguliwa rais wa Israel,na kujiuzulu katika bunge ambapo alikuwa ndiye kiongozi aliyehudumu kwa mda mrefu katika historia ya taifa hilo.
Alihudumu kwa miaka saba kama rais,kabla ya kujiuzulu mwaka 2014,akiwa rais mwenye umri mkubwa duniani.

No comments:

Post a Comment