Shimon Peres akimbizwa hospitalini baada ya kuugua
ghafla
- 14 Septemba 2016
Peres ameshika
nyadhifa nyingi serikalini
Aliyekuwa Rais wa tisa wa Israel ,
Shimon Peres , amekimbizwa hospitali iliyopo nje kidogo ya mji mkuu wa Tel Aviv
baada ya kuugua kiharusi.
Taarifa kutoka ofisi ya Perez
inasema kuwa amekuwa akipumua kwa msaada wa kifaa maalum.
Mnamo mwezi Januari mwaka huu Perez
alifanyiwa upasuaji mdogo wa moyo baada ya kuugua mshtuko wa moyo.
Image caption Peres alishinda tuzo
ya amani ya Nobel 1994 kwa kuongoza mazungumzo ya amani na Palestina
Msindi huyo wa tuzo ya nobel
ametimiza umri wa miaka 93 mwezi uliopita na amewahi kushikilia nyadhifa za juu
zaidi katika serikali ya Israel.
Aliachia madaraka ya urais mwaka
2004.
No comments:
Post a Comment